TAMASHA
la Serengeti Fiesta 2014, limefungwa rasmi juzi usiku katika viwanja
vya Leaders Club jijini Dar es Salaam huku likisindizwa na burudani
nzito kutoka kwa wasanii mbalimbali wa ndani na nje nchi wakiongozwa T.I
kutoka Marekani.
Shoo ya mwisho ya
tamasha la Serengeti Fiesta ambalo limedhaminiwa na kinywaji cha
Serengeti Premium Lager, lilivutia maelfu ya mashabiki waliofika
kushuhudia nyota wa muziki kama T.I, Davido, Naseeb Abdul 'Diamond
Platinum', Alikiba, Mwana FA, Stamina, Weusi na TMK wote wakitoa shoo ya
nguvu.
Katika viwanja hivyo
vyaLeaders ilikuwa ni gumzo na sehemu ya pekee kwa mashabiki waliofika
kushuhudia shoo ya aina yake kutoka kwa wasanii wa kimataifa.
Waliokuwa wa kwanza
kufungua shoo hiyo jukwaani walikuwa washindi wa Super Nyota wa msimu
uliopita, ambao walipagawisha vilivyo mashabiki.
Wasanii wa Tanzania
walistahili pongezi kwa kufanya shoo nzuri. Wasanii hao ni Mo Music,
Y-Tony, Makomando, Recho, Vanessa Mdee, Barnaba, Linah, Shaa, TMK
Wanaume Family, Tip Top Connection, Ommy Dimpoz na Ya Moto Band.
Hata hivyo umati
uliofurika viwanjani hapo ulipagawa zaidi, baada ya wasanii nyota kama
Micharazo kupanda jukwaani na nyimbo kama Baadaye na Kimya.
Stamina alishangiliwa
zaidi baada ya kudhihirisha kipaji chake kwamba yeye kweli ni msanii
bora wa miondoko ya muziki laini nchini. Wasanii wengine waliopagawisha
vilivyo ni pamoja na Mwana FA, Young Killa, Weusi, Ney wa Mitego kabla
ya Ali Kiba kutangaza kwa mashabiki kwamba mfalme arudi tena jukwaani.
Kiba alishangiliwa na mashabiki waliokuwa wakimfuatilizia wakati akiimba
wimbo wake wa Mwana Dar es Salaam.
Kabla ya T.I kupanda
jukwaani, Diamond na Davido waliwapagawisha vilivyo mashabiki na wimbo
waliouimba kwa kushirikiana wa My number one remix.
Muda uliokuwa
ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki ni wakati msanii bora duniani T.I
alipopanda jukwaani na kusababisha mashabiki kupiga makelele alipoanza
kupiga shoo.
T.I alishangaza
mashabiki vilivyo wakati alipotumbuiza nyimbo kama Whatever you like,
What you know, I’m never scared, Big shit poppin, Swagga like us, No
mediocre na Live your Life ambazo ziliwafanya mashabiki wapige mayowe
muda wote alipokuwa akitumbuiza.
T.I aliwashukuru
mashabiki na akawarudisha kidogo Afrika wakati alipoimba wimbo wa Ejeajo
ambao alishirikiana na P-Square, aliendelea kuwashukuru mashabiki wa
muziki wake nchini na kusema anatamani angekuja nchini kabla ya jana.
Akizungumza na
waandishi wa habari Meneja Chapa wa kinywaji cha Serengeti Fiesta,
Rugambo Rodney alimpongeza T.I kwa kuonesha shoo nzuri.
Rugambo alisema;
”Mwaka huu ziara ya Serengeti Fiesta ilikuwa na mafanikio makubwa na
kwamba imeweka historia baada ya kujivunjia rekodi zake katika matamasha
yaliyopita ya Serengeti fiesta nchini Tanzania.
"Nina furaha na kwa
niaba ya wenzangu, napenda kumshukuru kila mdau aliyefanikisha kufanyika
kwa tamasha hili…mashabiki, wasanii, vyombo vya habari, waandaaji,
hoteli na mawakala wote."
No comments:
Post a Comment