Madaktari wa Australia wamefanikiwa
kuwarejeshea uhai wagonjwa watatu baada ya kupandikizwa moyo uliokufa
katika operesheni ya kwanza kufanyika duniani.
Madaktari katika
hospitali ya St Vincent mjini Sydney walitumia dawa ya kuzuia kuharibika
iliyotengenezwa na Taasisi ya Utafiti wa Moyo ya Victor Chang kwa
kupandikiza viungo kwa Michelle Gribilas,mwenye umri wa miaka 57 na Jan
Damen mwenye umri wa miaka 44, huku mgonjwa wa tatu akiendelea kupona.Moyo mmoja, ulisimama mapigo kwa dakika 20 kabla ya kuurejesha katika uhai, ukiwa umewekwa katika mashine na kuuchoma dawa ya kuzuia kuharibika.
Jan Damen na mkewe Silvana |
Moyo unahuishwa baada ya kupoteza uhai na kupandikizwa. Hospitali hiyo inaamini asilimia 30 za watu watarejeshewa uhai kutokana na kugunduliwa kwa dawa hii, ambayo hupunguza kiwango cha uharibifu kwenye moyo na kuwa tayari kupandikizwa.
Michelle Gribilas (kushoto) Jan Damen(katikati) wakizungumza na daktari wao Kumud Dhital |
Dawa hiyo iliyochukua miaka 12 kuitengeneza, pia inasaidia kuimarisha kazi ya moyo ambao unatolewa baada ya kifo (DCD) wakati ukianzishwa kufanya kazi upya.
Bi Gribilas, ambaye amestaafu na kuishi Campsie kusini magharibi mwa Sydney, amesema ni mtu tofauti kwa sasa baada ya kupandikizwa moyo mpya.
No comments:
Post a Comment