Thursday 30 October 2014

Man city Hoi Capital one Cup waambulia kichapo

wachezaji wa man city wakijilaumu
Mechi za kombe la ligi ya CAPITAL  ONE CUP zimeendelea usiku wa kuamkia leo viwanjani.
Manchester City ikicheza nyumbani ilijikuta ikiwaduwaza mashabiki wake baada ya kukubali kichapo cha mabao 2 bila majibu kutoka kwa Newcastle utd na kutupwa nje kabisa ya mashindano hayo.
Nayo Tottenham hotspurs iliutumia vema uwanja wake wa nyumbani kwa kuichabanga vilivyo kabisa Brighton kwa jumla ya mabao 2-0.
Nayo Southampton ikairarua Stoke City kwa jumla ya mabao 3-2.
Kwa matokeo haya ya sasa, katika robo fainali Chelsea watapambana na Derby, wakati Tottenham watavaana na Newcastle utd. Nayo Liverpool itapepetana na Bournemouth huku Southampton ikikwaana na Sheffield utd.

No comments: