Wednesday, 29 October 2014

Wajerumani Sita wajumuishwa kwenye Tuzo Ya Ballon D'Or

Tuzo ya Ballon D`Or itatolewa Januari mwaka 2015 Kufuatia ushindi wa timu ya ujerumani katika kombe la dunia huko Brazil wachezaji wengi wa timu hiyo wameingia kwenye orodha hiyo inayojumuisha majina 23 ya wachezaji soka wa kimataifa.
Tuzo ya Ballon D`Or itatolewa Januari mwaka 2015
Wanasoka sita kutoka timu ya Ujerumani iliyopata ubingwa wa kombe la dunia mwaka huu huko nchini Brazil wameingia katika orodha ya walioteuliwa kuwania tuzo hiyo muhimu kabisa katika ulimwengu wa dimba,tuzo linalojulikana kama FIFA Ballon d'or zamani likiitwa tuzo la mchezaji bora wa mwaka.
Kufuatia ushindi wa timu ya ujerumani katika kombe la dunia huko Brazil wachezaji wengi wa timu hiyo wameingia kwenye orodha hiyo inayojumuisha majina 23 ya wachezaji soka wa kimataifa.Katika orodha ya wachezaji wa Ujerumani walioteliwa ni pamoja na magwiji kutoka timu ya Bayern Munich Bastian Schweinsteiger,Phillip Lahm,Manuel Nuer,Thomas Müller na Mario Götze sambamba na Toni Kroos aliyeihama Bayern Munich na kujiunga na Real Madrid ya Uhispania mnamo kipindi cha msimu wa joto mwaka huu.
Mchezaji wa Bayern Munich mholanzi Arjen Robben pia amefanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo pamoja na wachezaji wengine watano kutoka mabingwa wwa Champions Leaague Read Madrid ambao ni Gareth Bale,Karim Benzema Sergio Ramos,James Rodriguez na mshindi wa tuzo hiyo mwaka uliopita Cristiano Ronaldo.
Cristiano Ronaldo Mshindi wa tuzo ya Ballon D'or mwaka 2013Cristiano Ronaldo Mshindi wa tuzo ya Ballon D'or mwaka 2013
Nyota wa Argentina Lionel Messi ambaye ameinyakua tuzo hiyo mara nne pia ameorodheshwa mwaka huu pamoja na wanasoka wenzake kutoka timu yake ya Barcelona Andres Iniesta,Javier Mascherano na Neymar.Ama kwa upande wa tuzo inayotolewa kwa kocha bora zaidi wa mwaka wa FIFA,Kocha wa Ujerumani Joachim Löw ameteuliwa kuwania tuzo hiyo inayopiganiwa na makocha wengine 10 walioingia kwenye orodha hiyo,miongoni mwao akiwemo Kocha wa timu ya Bayern Munich Pep Guardiola na meneja wa timu ya soka ya taifa ya Marekani Jürgen Klinsmann.
Orodha zote hizo mbili za wachezaji na makocha waliotajwa kuwania tuzo hizo zimeandaliwa na wataalamu wa soka kutoka kamati ya FIFA pamoja na gazeti la michezo la Ufaransa.Mshindi wa mwisho atachaguliwa na manahodha wa soka pamoja na makocha wa timu za taifa sambamba na wawakilishi wa vyombo vya habari vya Kimataifa mnamo Tarehe 12 mwezi Januari mwaka 2015 huko Zurich Uswisi.
wengine waliomo katika orodha hiyo ni pamoja na mcheazji wa Cote d´Ivoire Yaya Toure anayelisaka dimba Manchester City katika ligi kuu ya England, Premier League , Zlatan Ibrahimovic kutoka Sweden anayechezea PSG ya Ufaransa na Angel Di Maria wa Argentina kutoka kilabu ya Manchester United ya Uingereza.

No comments: