Bondia
Pungluang Sor Singyu wa Thailand kushoto akipambana na Fadhili Majiha wa
Tanzania wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Dunia WBO Asia
Pacific bantamweight title uliofanyika katika uwanja wa shule ya
Amphawa iliyopo Bangkok, Thailand Majiha alipigwa kwa point
Bondia Fadhili
Majiha wa Tanzania kushoto akipambana na Pungluang Sor Singyu wa
Thailand wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Dunia WBO Asia
Pacific bantamweight title uliofanyika katika uwanja wa shule ya
Amphawa iliyopo Bangkok, Thailand Majiha alipigwa kwa point.(P.T)
Na Mwandishi Wetu
BONDIA nambari moja kwa ubora nchini Tanzania katika uzito wa bantamweight
Fadhili Majiha 'Stoper' mwishoni mwa wiki iliyopita alikuwa na kibarua
kizito kutoka kwa Mthailand aliyemenyana nae nyumbani kwao Thailand na
kupigwa kwa point.
Akizungumzia
matokeo hayo ya kupigwa kwa point bondia huyo amejigamba na kusema kuwa
yeye alistaili ushindi hivyo wamempa kwa kuwa kacheza kwao na mcheza
kwao utunzwa mana nilicheza kwa ustadi wa ali ya juu na wapenzi wote wa
ngumi walikuwa upande wangu wakitafakali kwa nini nilinyimwa ushindi bondia
huyo ambaye anatamba sana hapa nchini kuwa hakuna wa kumbabaisha ambapo
anadai kukimbiwa mara mbili na bondia Fransic Miyeyusho pamoja na
Nassibu Ramadhani ambao wote amewapa onyo ole wake mmoja wao akaingia
anga zake atakiona cha moto kwa kuwa mechi zao nyingi wanapenda
kupangiana wenyewe kwa wenyewe.
Nimerudi
nyumbani nipo fit sina ata kovu la aina yoyote hile hivyo nitahakikisha
nafanya mazoezi kuendeleza ufiti niliokuwa nao na napenda kutoa
tahadhali kwa bondia yoyote mtanzania atakayejitokeza kwa sasa mbele
yangu yeye atakuwa halali yangu.
Nae Kocha
wake Waziri Chara amejigamba kwa kusema kuwa bondia wake ni wa
kimataifa ambapo michezo yake karibia mitatu kacheza Philippines na
mwingine Thailand hivyo wao ni wa kimataifa zaidi mana mapambano
aliyocheza nje yote yalikuwa magumu na raundi ni 12 ambapo zote
alimaliza kwa kuwa nilimjenga katika mazingira mazuri mabondia wengi
wakienda nje ya nchi wengiwao wanapigwa raundi ya kwanza ya pili awafiki
ya nne
No comments:
Post a Comment