Mchungaji Libby Lane
KANISA moja la Kianglikana nchini Uingereza
limemuapisha mwanamke wa kwanza kuwa kasisi. Mchungaji Libby Lane
ameapishwa katika sherehe iliofanyika eneo la York Minster, na atakuwa
Kasisi wa Stockport ikiwa ni miezi sita tu baada ya kanisa hilo kumpigia
kura ili kumaliza utamaduni wake wa wanaume kuwa makasisi.
Kasisi huyo alisema kuwa iwapo uchaguzi wake utawafanya wanawake
kubaini uwezo wao basi anafurahia. Hatua hiyo imeendelea kuzua hisia
tofauti miongoni mwa wafuasi wa kanisa hilo la kianglikana duniani.
No comments:
Post a Comment