Waendesha mashtaka nchini Marekani wamewafungulia mashtaka raia wa tatu
wa Marekani kwa kuhusika kwenye njama ya mapinduzi nchini Gambia.
Alagie
Barrow aliye na uraia wa Marekani na Gambia alifikishwa mahakamani
kwenye jimbo la Minnesota akikabiliwa na mashtaka ya kuendesha harakati
za kijeshi dhidi ya nchi rafiki.Taarifa ya mahakama ilisema kuwa bwana Barrow alishukiwa kusaidia kupanga mapinduzi hayo.
Mapinduzi hayo yalifeli wakati walinzi wa rais walipowafyatulia risasi wale waliojaribu kuendesha mapinduzi hayo ambayo baadaye walisafiri kwenda nchini Marekani ambapo walikamatwa.
No comments:
Post a Comment