Mfanyabiashara
na mmiliki wa duka la dawa katika eneo la Mrombo Arusha Bi elizabeth
mshana akiongea na Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde juu ya huduma
ya kufanya malipo kwa kutumia kadi ya Airtel Money Near Field
Communication (NFC) based solution ya Airtel Money. kadi hii maalum
inamuwezesha mteja kufanya malipo kwa haraka kwa kugusisha kwenye kifaa
maalum tu mara moja, kisha kuweka nambari ya siri na kufanya malipo
mahali popote. kwa sasa huduma hii imeanza kufanya kazi mkoani Arusha.
Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) yaani kulipa kwa kugusisha
kadi na kifaa tu kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni
yakwanza kuzindulia nchini na kampuni ya simu za mkoni ya airtel.
Mama
elizabeth mshana mmiliki wa duka la dawa akimuuzia mteja dawa kwa
kupitia kadi huduma iliyozinduliwa na Airtel mkoani Arusha
inayowawezesha wateja wake kufanya malipo kwa haraka zaidi kwa kutumia
kadi hiyo maalumu ya airtel Money yenye teknolojia ya Near Field
Communication (NFC) based ikiwa imeunganishwa na Airtel
Money.akishuhudia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde. Huduma hii
ya Near Field Communication (NFC) kupitia huduma za kifedha kwa njia ya
mtandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni yasimu za mkoni ya
airtel.
Afisa
uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya AIRTEL Jane Matinde
akimuelekeza Moja ya wateja bi Merry Ngowi jinsi ya kutumia kifaa na
kadi maalumu ambacho hutumika kukamilisha miamala ya malipo katika
maduka mbalimbali. Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) kupitia
huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ni yakwanza kuzindulia nchini na
kampuni ya simu za mkoni ya airtel, tukio lifanyika mwishoni mwa wiki
mkoani arusha eneo la muromboo wakati wa uzinduzi huduma hiyo ambayo
inaleta njia salama, ya haraka na rahisi kwa wateja kufanya malipo.
Mfanyabiashara
wa duka la chakula katika eneo la Mrombo Arusha Bwana Elibariki Ngowi
akipokea malipo kutoka kwa mteja kwa kupitia kadi maalum ya Near Field
Communication (NFC) ya Airtel Money. , huduma imezinduliwa na Airtel
mkoani Arusha inawawezesha wateja wake kufanya malipo kwa kutumia kadi
hiyo maalumu kwa haraka bila huanza kupiga *150*60# hii unagusisha tu na
kulipa haraka kati kanti ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde
akishudia huduma hiyo inavyofanya kazi. Huduma hii ya Near Field
Communication (NFC) kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni
yakwanza kuzindulia nchini na kampuni ya simu za mkoni ya airtel.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel leo (mwishoni mwa wiki) imetangaza huduma
ya kwanza sokoni inayotumia kadi maalumu kwa kupitia huduma ya Airtel
Money. Huduma hiyo mpya inayowawezesha wateja wa Airtel Money kufanya
malipo kwa kutumia kadi imeanza katika mkoa wa Arusha na itaendelea
kufikishwa katika mikoa mbalimbali nchini.
Akiongea
kuhusu huduma hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Money Aijaza Khan alisema"
technologia inakuwa kwa kasi na tumeonelea ni muhimu kwenda sambamba na
mabadiliko hayo kwa kuleta huduma za kibunifu zitakazokithi mahitaji ya
wateja wetu yanayokuwa kwa kasi kila siku. Nia yetu ni kuona wateja wetu
wanapata huduma za kisasa kwa wakati wote. Huduma hii mpya
tunayoitambulisha leo itawawezesha wauzaji na wanunuzi kupata njia
rahisi, ya uhakika na salama ya kufanya miamala na malipo yao ya kila
siku. ili kutumia huduma hii kila mteja atatakiwa kupata kadi maalum
inayomuwezesha kufanya malipo kirahisi , kwa haraka na kwa usalama
katika maduka mbalimbali yaliyopatiwa vifaa maalumu kwaajili ya kupokea
malipo toka kwa wateja. Huduma hii imeshaanza kufanya kazi kwa
wafanyabiashara na wateja wetu Arusha.
"Kadi hii
maalumu imeunganishwa na akaunti ya Airtel Money ya mteja, mteja
anachotakiwa ni kugusisha kadi yake na kifaa cha kupokea malipo (POS)
ili kuweza kufanya malipo. Malipo yatakamilika pale mteja
atakapothibitisha muamala kwa kuweka namba yake ya siri kwenye kifaa cha
malipo
Tunajivunia
kuwa mtandao wa kwanza Tanzania kuanzisha huduma hii ya kibunifu
itakayowawezesha wateja wetu kufanya malipo ya kwa urahisi, haraka ,
kiusalama bila kuwa na haja ya kupiga namba ya Airtel money na kuingia
kwenye orodha, Kwa kutumia kadi maalumu mteja anaweza sasa kufanya
malipo. ". aliongeza Khan
Akiongea
kuhusu faida za huduma hiyo , Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde
alisema" huduma hii inafaida nyingi kwa wafanyabishara na wateja ikiwa
ni pamoja na njia salama ya kuifadhi pesa, ya kuhakiki na kukusanya
pesa,mfanyabiashara anaweza kuzipeleka moja kwa moja benki kutoka kwenye
kifaa hicho au kutoa pesa kwa wakala aliye karibu. Kwa upande wa wateja
faida hizo ni pamoja na kufurahia urahisi, usalama, uharaka wa kufanya
malipo na pia kuepusha wateja kutembea na pesa nyingi mfukoni ili
kufanya malipo. Mteja atakapopoteza au kuibiwa kadi yake pesa zake
kwenye kadi yake zinabaki salama aliongeza" Matinde
Akiongelea
kuhusu uzoefu alioupata a kutumia huduma hii ya kadi kupitia Airtel
Money, Mfanyabiashara na milliki wa Phamarcy Bi Elizabeth Mshana
alisema" Huduma hii ni ya kipekee na imerahisisha sana namna ya kufanya
biashara maana ni rahisi kutumia na ni salama. Wateja wanapokuja dukani
kununua dawa na hawana pesa taslimu mfukoni wanatumia huduma hii na mimi
kama muuzaji nafurahi kwakuwa pesa zangu ziko salama na sina haja ya
kufikiri kuhusu kutafuta chenji. Kwa kweli ni huduma nzuri na
tunaifurahia na nawashauri wafanyabiashara wenzangu na wateja kutumia
huduma hii kwani inaleta ufanisi"
Huduma
hii inapatikana sehemu mbalimbali ikiwemo maduka ya biadhaa , maduka ya
chakula, maduka ya dawa, mawakala wa Airtel Money na Baa, Mpango mkakati
ni kufikisha huduma hii katika maeneo mbalimbali nchini kwa mwaka huu.
Airtel
kupitia huduma yake ya Airtel Money hivi karibuni imezindua huduma
nyingine ya kibunifu ijulikanayo kama Timiza inayowawezesha wateja wake
kupata mikopo rahisi papokwa papo na kurejesha baada ya wiki moja au
mwenzi huduma ambayo imewawezesha watanzania wengi kuboresha mitaji ya
biashara zao na kutatua changamoto ndogondogo za kila siku.
No comments:
Post a Comment