Watu wenye silaha wasiofahamika walimfyatulia risasi na kumuuwa
mchungaji mmoja wakati wa ibada kanisani siku ya jumapili katika mji wa
Mombasa nchini Kenya maahala ambako polisi wanapambana na vijana wa
ki-islam wenye msimamo mkali.
Mauaji hayo yalitokea ndani ya mlango mkuu wa kuingilia kwenye kanisa
la Maximum Revival Centre katika mtaa wa majengo. Mashahidi wanasema
polisi waliwazuia watu wenye silaha kuingia ndani ya kanisa na kuuwa
waathirika Zaidi.
Watu hao wenye silaha hawajafahamika lakini kundi la wanamgambo wa
Al-Shabab kutoka nchi jirani ya Somalia limeshambulia malengo kadhaa
nchini Kenya. Kundi hilo la Al-Shabab liliapa kulipiza kisasi kwa
majeshi ya Kenya kuwepo nchini Somalia kwa ajili ya kusaidia wanajeshi
wa serikali dhidi ya wanamgambo hao.
No comments:
Post a Comment