Askofu
mmoja nchini Nigeria ametoa wito kwa mataifa ya magharibi kufanya
juhudi za kutosha dhidi ya Boko Haram kama ilivyofanywa dhidi ya
washambuliaji wa kiisilamu nchini Ufaransa.
Askofu Ignatius Kaigama amesema mataifa ya magharibi yanapuuza sana tisho linalotokana na Boko Haram kwa watu wa Nigeria.Askofu huyo wa Jos, aliongeza kwamba rasilimali zote zinatakiwa kutumika ili kuzuia juhudi za kundi hilo kukita mizizi nchini Nigeria. Pia amesema kwamba dunia inapaswa kuonyesha ari ya kutaka kuangamiza kundi hilo.
Kadhalika askofu huyo amesisitiza kwamba mauaji ya hivi karibuni ya mamia ya watu mjini Baga ni ishara kwamba jeshi la nchi hio limeshindwa kukabiliana na wapiganaji hao.
Onyo la askofu huyo linakuja siku mbili tu baada ya mashambulizi ya bomu kuwaua zaidi ya watu 20.
Mnamo Jumapili,washambuluaji wawili wa kike walifanya mashambulizi ya kujitoa mhanga na kuwaua watu wanne huku wnegine zaidi ya arobaini wakijeruhiwa mjini Potiskum
Siku moja kabla ya mashambulizi hayo, mashambuluaji mwingine w akujitoa mhanga alishambulia mji wa Maiduguri na kuwaua watu 19.
Mashambulizi haya yametokea baada ya taarifa kwamba mamia ya watu waliuawa wiki jana wakati Boko Haram ili poteka mji wa Baga katika jimbo la Borno
SOURCE: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment