Friday 16 January 2015

Mbunge wa Viti Maalum CCM Iringta Mjini Ritta Kabati amewataka wakinamama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu

Mbunge wa viti maalumu Iringa mjini RITTA KABATI

Mbunge wa viti maalumu Iringa mjini RITTA KABATI  amewataka wakinamama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
 
KABATI ameeleza kuwa wanawake waondoe hofu ya kugombea hasa kukiwa na ushindani wa wagombea wanaume kwa kuogopa kuchafuliwa kwa mambo yasiyokuwepo.
Ameendelea kusema kuwa wananchi wasishawishiwe na propaganda za wanasiasa na badala yake wachague viongozi bora wenye uwezo wa kuongoza kutoka katika chama chochote.
Aidha ameongeza kuwa viongozi wawe na sera za kutekelezeka ili kuwatendea haki wapiga kura wao hali itakayowafanya waaminike katika jamii.
KABATI amesema kuwa wanawake wawemstari wa mbele kuchukua fomu za kugombea na kwamba wasikatishwe tamaa na baadhi ya watu wanaodhani kwamba wanawake hawawezi kugombea na kuongoza katika nafasi mbalimbali.
Aidha ameongeza kuwa Jamii iachane na mitazamo tofauti kwa wanawake wanao jitokeza kugombea nafasi za uongozi na kuwaasa wanawake wawe na misimamo pindi wanapoingia madarakani, kujiamini na kutokubali
kutumiwa kama chombo cha starehe.
Mbali na hayo KABATI amewakumbusha vijana kutokubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa katika kuleta vurugu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na badala yake wachague kiongozi mwenye weredi na sifa za kuwa kiongozi kutokana na sera za chama chake.
Ameendelea kusema kuwa vijana wajotokeze kwa wingi katika kupiga kura ndiyo katika katiba iliyopendekezwa ili kuweza kufanya uchaguzi ulio wa haki na amani pia kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura pamoja na kupiga kura.

No comments: