Vijana wanaocheza michezo ya video |
Mtu
moja mwenye umri wa miaka 32 huko Taiwan amefariki baada ya kucheza
michezo ya mitandaoni,ikiwa ni kisa cha pili kwa mchezaji kama huyo
kuaga dunia.
Imebainika kuwa mtu huyo aliaga dunia masaa kadhaa huku wenzake wakiendelea kucheza bila kujua.Alipatikana amelala katika meza moja ndani ya mgahawa wa mitandao mnamo Januari 8 akiwa hana uhai na kulazimika kupelekwa hospitalini ambapo alitangazwa kwamba amefariki.
Vijana wakicheza michezo ya mitandaoni |
Maafisa wa Polisi wamesema kwamba wachezaji wa mchezo wa mtandao katika mgahawa huo waliendelea kucheza bila kugundua ni nini haswa kilichotokea licha ya maafisa hao pamoja na madktari kuwasili ili kumchunguza mtu huyo.
No comments:
Post a Comment