Wenyeji Equitorial Guinea waliandika bao la kwanza katika dakika ya 55 kipindi cha pili kwa mkwaju wa penalti baada ya Lloyd Palun kufanyiwa faulo katika eneo la hatari.
Kama hiyo hatoshi Wenyeji hao wakapigilia msumari wa moto kwenye kidonda pale waliondika bao la pili kupitia Salvador Iban ambaye aliukwamisha mpira wavuni uliotemwa na mlinda mlango wa Gabon.
Nayo Congo Brazavile ambayo ilihitaji sare ya aina yoyote ili isonge mbelehatua ya robo fainali ilipata goli lake la kwanza kupitia kwa mchezaji Thierry Bifouma huku goli la pili likifungwa na Fabrice Ondama.
Goli pekee la Burkina Faso lilitiwa wavuni na Aristide Bance.
Kwa matokeo hayo Congo Brazaville inaingia hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa mara kwanza tangu mwaka 1992.
Leo kutakuwa na mechi mbili za kundi B ambapo timu mbili kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na kati Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia zitatupa karata zao za mwisho ambapo Jamuhuri Kidemokrasia ya Kongo itaumana vikali na Tunisia huku Zambia ikikutana uso kwa uso na Cape Verde.
Zambia na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lazima zishinde mechi zao leo ili ziweze kusonga mbele hatua robo fainali huku Zambia ikihitaji ushindi wa magoli zaidi ya matatu kwa bila.
No comments:
Post a Comment