Mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA imefuta usajiri wa aina za
dawa za binadamu aina tano na kuamuru ziondolewe sokoni na vituo vyote
vya kutolea huduma za afya mchini kote mara moja kutokana na kubainika
kuwa na viambata vinavyosababisha maradhi sugu ikiwemo kiharusi, na
wakati mwingine kusababisha vifo.
Dawa zinazotajwa kufutiwa usajiri na kuzuia uingizwaji kuwa ni
pamoja na dawa za kutibu maralia ya maji na vidonge aina ya Amodiaquine,
dawa za kutibu mafua na kikohozi za maji, vidonge na kapsulis zenye
kiambata cha Fenil Propanolamine nyingine ni dawa ya sindano aina ya
Chloramphenical inayotengenezwa na kiwanda cha Lincoln cha nchini India,
dawa za kutibu fungus ya vidinge na kapsuli.
Akitangaza dawa hizo mkurugenzi mkuu mamlaka ya chakula na dawa
TFDA Bw. Hiit Sillo hatua hiyo imefikiwa baada ya uchuguzi wa kitaalam
wa muda mrefu kwa kutumia mifumo ya ufuatiliaji wa usalama na ubora wa
dawa ambao pia unafanya kazi kwa kutumia mtandao wa kimataifa kwa
ushirikiano wa shirika la afya duniani WHO.
Aidha TFDA imefanya mabadiliko ya matumizi ya dawa ya maralia ya SP
kutumika kama kinga ya maralia kwa wanawake wajawazito tu na kuagiza
watengenezaji kubadili machapisho na vifungashio vyake mara moja ambapo
mkurugenzi wa dawa TFDA Bw. Mitanga Fimbo pamoja na kufafanua athari
anawataka watoa huduma nchini kote kuondoa dawa hizo na kuziteketeza
mara moja kabla ya kuanza kwa msako.
No comments:
Post a Comment