Sunday, 18 January 2015

watano wafa katika maandamano Nigeria

Maandamano Niger
Watu watano wameuawa kwenye mji mkuu wa Niger, Niamey ikiwa ni siku ya tatu ya maadamano ya kupinga kuchapishwa kwa kibonzo cha mtume Mohammed na gazeti la kila wiki nchini Ufaransa la Charlie Hebdo.
Karibu vijana 1000 waliokuwa wamebeba chuma na shoka waliandamana kwenye barabara za mji huo wakiwarushia polisi mawe ambapo walijibu kwa kurusha vitoa machozi.
Waandamanaji hao walichoma moto karibu makanisa 7 mjini Niamey.
Maiti mbili zilizokuwa zimekatwakatwa zilipatikana ndani ya kanisa moja lililokuwa limeteketezwa moto.
Picha za runinga zilionyesha waandamanaji wakirarua biblia wakisema Allahu Akbar huku wakipeperusha Koran.
Baadhi ya biashara za Ufaransa nazo zilivamiwa yakiwemo maduka ya kampuni ya simu ya Orange.
Ubalozi wa Ufaransa nchini humo umewashauri raia wake walio mjini Niamey kusalia majumbani mwao.

No comments: