Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Wakati alipokuwa klabuni Simba SC
alikataa kufananishwa na aliyekuwa ‘ staa’ wa timu hiyo, Mussa Hassan
Mgosi kwa madai kwamba mchezaji huyo wa zamani wa timu Taifa, Taifa
Stars alikuwa ba ubora mkubwa kuliko yeye. Namzungumzia, Mbwana Samatta ‘
kipaji cha hali ya juu kutoka Tanzania. Samatta aliichezea Simba kwa
miezi minne na kufunga mabao nane katika ligi kuu na mengine matatu
katika klabu bingwa Afrika kabla ya kununuliwa kwa dau la dola 100, 000 (
zaidi ya milioni 150) na klabu bingwa mara nne ya kihistoria Afrika, TP
Mazembe katikati ya mwaka 2011.
Mfungaji huyo bora wa Kombe la
shirikisho Afrika, 2013 kwa sasa yuko katika majaribio na kuna uwezekano
mkubwa akasajiliwa na CSKA Moscow ya Urusi. Kama mambo yatanyooka kama
tunavyohitaji Watanzania wengi, Samagoal, anaweza kucheza ligi ya
mabingwa barani Ulaya msimu ujao. Kitendo tu cha kupata mwaliko kutoka
kwa timu hiyo iliyocheza ligi ya mabingwa hatua ya makundi msimu huu ni
hatua kubwa lakini hataishia hapo kwa kuwa ni kijana mwenye hitaji kubwa
katika soka.
Wakati alipotua TP, Samatta
alikutana na changamoto nyingi, lakini kubwa ilikuwa ni kitendo cha
mashabiki wengi wa TP kumuweja juu na kumchukulia ‘ mchazaji wao bora
klabuni’. Bahati ni kwamba nimekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na
Samatta kiasi cha kufahamu baadhi ya changamoto anazokutana nazo katika ‘
soka la kulipwa’. Kuna wakati niliwahi kufanya naye mahojiano wakati
huo akiwa katika mwaka wake wa kwanza, TP, nilimuuliza mengi lakini
kubwa nilihataji kujua kuhusu ‘ ulinganisho wa mashabiki kuhusu yeye na
Tressor Mputu.
Kama alivyokataa kulinganishwa na
Mgosi, ni hivyo pia Samagoal aliniambia, ‘ Sifanani na Tressor, yeye
tayari ana tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika’. Hata kama ndani ya uwanja
mashabiki waliona ubora wa Samatta kuliko Mputu, yeye mwenyewe (
samatta) aliendelea kujifunza na kujenga mahusiano mazuri zaidi ya ndani
na nje ya uwanja na Tressor huku akichukulia kitendo cha kucheza timu
moja na mchezaji huyo bora wa Afrika, 2009 kwa wachezaji wa ndani ni
jambo la heri na kujivunia.
Wakati akitua TP, timu hiyo
ilikuwa na washambuliaji, Tressor na Given Singuluma lakini juhudi
binafsi ikiwemo kukubali kucheza nje ya nafasi aliyoizoea kulimfanya
Samatta kupata nafasi kikosi cha kwanza huku mabao yake sita katika ligi
ya mabingwa Afrika, 2012 yakimpatia nafasi ya kupangwa sambamba na
Tressor katika safu ya mashambulizi na Mzambia, Singuluma akawa akicheza
eneo la kiungo. Samatta alipenya taratibu katika kikosi cha kwanza, TP
lakini bado alikuwa na ‘ usongo’ uleule. Upi huo?.
Miaka minne iliyopita alisema, TP
ni njia tu, kituo kipo Ulaya. ; “ Kwa kweli nakosa mpaka maneno
ya kumuelezea, ila nabaki kuamini kuwa Mungu ana baraka zake. Sijapata
kufikiria kama kipaji kile ni mdogo wangu wa kuzaliwa tumbo moja, katika
vipaji ambavyo vipo duniani Mbwana ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa na
namuweka katika orodha ya wachezaji 20 bora wenye vipaji vikubwa
duniani. Kwa sababu ni Mtanzania anaweza kuonekana ni mchezaji wa
kawaida, lakini kile ni kipaji maridhawa ambacho nimewahi kukiona. Ndiye
mchezaji ambaye namkubali sana nchini. Ni kipaji ambacho ametunikiwa na
Mungu. Nina imani atakuwa mbali sana akicheza mpira wa kulipwa ulaya,au
la basi anaweza kuwa mchezaji anayelipwa zaidi Africa kama ataongeza
mkataba pale TP Mazembe” anasema Mohamed Samatta mchezaji wa JKT Mgambo
na kaka wa Mbwana.
Hata kabla ya ofa ya CSKA,
Samatta amekuwa mtulivu, mvumilivu, na kmiakkiwa na kijana msikivu
mwenye ndoto kubwa. Amefanikiwa kwa kiasi chake na wakati huu umri wa
miaka 21, Ulaya ni kituo muhimu alichopanga kufika. Hana makuu licha ya
kuwa staa wa kweli katika soka la DRC, Afrika na kitendo cha kuwaheshimu
wachezaji kama Mgosi na Tressor wakati akitengeneza jina kimechangia
mafanikio hayo sasa kuna nafasi kubwa ya Mtanzania huyo kucheza sambamba
na Zoran Tosic, mshambulizi wa Serbia ambaye Sir Alex Ferguson alitoa
pauni 17 milion na kumpeleka Manchester United katikati ya mwaka 2008.
Labda inaweza
kutokea siku Mbwana Samatta akacheza ligi ya mabingwa ulaya, kwani CSKA
Moscow ni timu ya mara nyingi katika michuano hiyo na msimu huu
wameondolewa katika hatua ya makundi baada ya kumaliza nyuma ya FC
Bayern Munich, Manchester City na AS Roma. Inaweza kuwa ndoto ya kweli,
ni jambo la kusubiri na kuona kabla ya ili kuona kama kweli, Samagoal
ataingia tena katika ushindani wa namba na Zoran, baada ya kufanikiwa
dhidi ya Mgosi na Tressor huku akiwapa heshima kubwa.
“ Nachoweza
kusema nimekuwa makini na mtulivu, na wakati mwingine huwa nasema ni
bahati kutoka kwa Mungu. Mimi ni ‘ mwanajeshi wa mbele’ mshambulizi wa
kwanza kabisa, hivyo ndivyo ninavyotumika katika klabu yangu na nimekuwa
nifunga mabao ya kutosha kutokana na kupangwa katika nafasi hiyo
nayoipenda. Mchezaji huwezi kujichagulia nafasi ya kucheza katika timu,
mahitaji ya Mwalimu ndiyo jambo la msingi. Napenda kucheza katika nafasi
yoyote nayopangwa kutokana na mfumo wa kocha anavyotaka” anasema
Samatta
No comments:
Post a Comment