Friday 7 February 2014

Al-Sissi atangaza kugombea urais

MKUU wa majeshi nchini Misri, Abdul-Fattah al-Sissi, amesema katika maelezo yaliyochapishwa jana na gazeti la Al-Seyassah nchini Kuwait, kwamba ameamua kugombea katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Aprili.
Gazeti hilo limemnukuu al-Sissi akisema suala hilo limekwishaamuliwa na kwamba hana njia nyingine zaidi ya kuitikia wito wa raia wa Misri.
Kwa mujibu wa DW, ripoti hiyo inakuja wiki moja baada ya Baraza Kuu la Kijeshi nchini humo kumuidhinisha Jemedari al-Sissi kugombea katika uchaguzi huo.
Bw. Al-Sissi ana uhakika wa kushinda, baada ya kumpindua rais aliyechaguliwa kidemokrasia, Mohammed Mursi, Julai mwaka jana.

No comments: