Wednesday 5 February 2014

Rio bado ni mchezaji mwenye thamani man u


KOCHA wa Manchester United, David Moyes,
amesisitiza kwamba bado anamchukulia Rio
Ferdinand mchezaji mwenye thamani Old Trafford.
Nahodha huyo wa zamani wa England amekuwa
akisumbuliwa na majeraha msimu huu, akifunikwa na Jonny Evans na Phil Jones huku akiwa amecheza mechi
saba tu za ligi.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Goal, Moyes amesema Ferdinand anaweza kurudi kikosi cha kwanza Jumapili dhidi ya Fulham .
"Rio anafanya mazoezi," Moyes aliwaambia waandishi wa habari na kuongeza, "amerudi na tutaendelea kumtumia Rio kwa wakati mwafaka.
"Ametoa mchango mkubwa, hasa katika nusu ya kwanza ya msimu. Ni kweli ana ushindani katika nafasi yake, lakini anathaminiwa sana na kuangaliwa kama mmoja wa wachezaji waandamizi hapa," alisema Moyes

No comments: