Wednesday, 5 February 2014

Ujerumani watishia kuwawekea ikwazo vya kiuchumi Ukraine

UJERUMANI imeelezea uwezekano wake mkubwa wa kuuwekea vikwazo uongozi wa Ukraine.
Kwa mujibu wa DW, uamuzi wa Ujerumani ni kama njia ya kufanikisha ushiriki wa majadiliano na upinzani na kutatua mgogoro wa kisiasa wa taifa hilo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani , Frank- Walter Steinmeier, amesema vikwazo dhidi ya Ukraine kwa sasa visiangaliwe kama kitisho.
Kauli ya waziri huyo imetolewa wakati Uingereza na Marekani zikisema ziko tayari kuzungumzia msaada wa fedha ikiwa suluhisho la kisiasa litafikiwa.
Ukraine imekumbwa na machafuko tangu Novemba, mwaka jana, baada ya Rais Viktor Yanukovich kukataa mkataba wa makubaliano ya kibiashara ya Umoja wa Ulaya.
Hata hivyo, Rais Yanukovich na badala yake aliukubali msaada wa fedha kutoka Urusi kuuokoa uchumi wake.

No comments: