
Wasichana wadogo nchini Kenya wamekuwa wakilazimika kujiingiza katika
unywaji pombe na uuzaji wa miili yao kama njia ya kujipatia chakula wao
na familia zao.
Brittanie Richardson binti wa kimarekani mwenye umri wa miaka 27
ameanzisha kampeni ya kupinga hali hiyo baada ya ziara yake
iliyoshuhudia vitendo hivyo vya mara kwa mara kwa familia zilizo na hali
ngumu ya maisha.
Mjini Nairobi kuna msongamano mkubwa wa makazi duni, watoto wenye njaa
mara nyingi wanafanya biashara ya miili yao ili kujipatia pesa kidogo au
chakula, mji huo wenye wakazi milioni 3.1, ni nyumbani kwa watu milioni
2 wanaoishi katika makazi duni na idadi ya watu katika makazi duni
katika mji huo mkuu wa Kenya inakua kwa asilimia 6 kwa mwaka.
 |
Eneo la fukwe za utalii nchini Kenya |
Kulingana na shirika la kuwahudumia watoto la umoja wa Mataifa
Kenya ina watoto wanaofanya kazi ya ngono 30,000 waliogawanyika katika
pembe zote za fukwe za utalii, huku ukahaba miongoni mwa watoto
likitambuliwa kama tatizo linalohitaji kukabiliwa kwa utekelezaji wa
sheria kali na kuwapa wasichana hao ncji mbadala ya kujikwamua kutokana
na mtego huo.
Richardson kutoka mji wa Atlanta, katika jimbo la Georgia nchini
Marekani hakuwa na wazo juu ya kiwango cha tatizo nchini Kenya mpaka
pale aliponza kusafiri mara kwa mara Afrika wakati akiwa chuoni. Awali
alikuwa akisaidia nchi ya Afrika Kusini kupambana na kukosekana haki ya
kijamii na kisha nchini Msumbiji.
Mkutano na mwanamke wa Canada nchini Msumbiji ambaye alihitaji msaada wa
kuanzisha makaazi ya kuwaokoa watoto walionasa katika ukahaba,
ulimfanya Richardson kuelekea katika mji wa Mtwapa nchini Kenya, ambao
umekuwa na sifa mbaya ya ukahaba katika eneo la pwani.
Richardson alisema, na hapa ninamunukuu, "Ulikuwa ni wakati wa
kuhuzunisha na kushitusha kuona binti wa miaka 15 kiasi kidogo mwenye
miaka minane akiinieleza kuwa analazimika kufanya ngono ili aweze kupata
chakula kiukweli nilishituka.
Richardson alijiona yeye mwenyewe nakuwa mmoja wa watu wanaongoza
harakati za kuendesha kampeni ya ngazi za chini kupambana na umasikini
kuacha kuwapeleka watoto wanaotoka katika makazi duni katika biashara ya
ngono.
 |
Uwanja wa ndege wa Kimataifa Kenya |
Lakini baada ya miaka miwili ya harakati za kituo cha Mtwapa,
Richardson anataka kufanya kazi zaidi ya kusaidia na mwezi wa nne mwaka
huu aliweka kitengo cha sanaa na kukomesha unyanyasaji chenye lengo la
kusaidia watumwa wa ngono kupitia kufanya sanaa ambayo anaona itakuwa
tiba na dawa.
Kwa kusaidiwa na mfanyakazi wa kijamii, Richardson aliwachagua wasichana
10 wenye umri kati ya miaka minane na 16 waliokuwa wakiishi katika
makazi duni ya Sinai kuwa sehemu ya mpango wake. Sinai ni moja ya makazi
200 duni mjini humo.
Richardson alisema Kati ya wasichana hao 10 kati yao ama wamebakwa au
wamelazimishwa na umasikini au wazazi wao kufanya ngono ili kujipatia
fedha Aliongeza kuwa majukumu yake katika kazi hiyo inatokana na uzoefu
wake kutokana na kufanyiwa unyanyasaji wa kingono wakati wa utoto wake
na ndugu wa karibu katika familia yake lakini kila mtu amejaribu kupuuza
jambo hilo.
Anaipongeza asasi ya vijana ya michezo ya kuigiza ya Freddie Hendricks
ya mjini Atlanta, iliyoanzishwa na mwanamuziki wa muziki wa miondoko ya
jazz kwa kuyaokoa maisha yake. Alisema aliona upendo wa kweli
waliomuonyesha kama mwathirika na anataka kufanya vivyo hivyo kwa
wasichana wengi.
Lakini kazi yake itafanikiwa kwa gharama na Richardson ameweza
kufanikisha uungwaji mkono kutoka idadi kubwa ya wasanii, wanaharakati
mjini New York ambao wamekuwa wakiendesha jitihada za kuchangisha kwa
ajili ya onyesho lenye kupinga na kukemea vitendo vya unyanyasaji wa
ngono dhidi ya wasichana.