Aidha alisema katika tukio la kurushiwa mawe mlinzi wake, Abdallah
Mazengo alipigwa jiwe kichwani na kuzimia kwa masaa kadhaa, hata hivyo
hali yake inaendelea vizuri.
KAMANDA wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas, amesema kuwa tuhuma
alizotoa Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema si za kweli.
Kamanda huyo alisema madai kwamba polisi wanamuonea Lema kwa
kumkamata na kumweka mahabusu wakati yeye siyo mhalifu siyo za kweli na
kwamba yeye (Lema) ni chanzo cha vurugu katika uandikishwaji wa daftari
la wapigakura.
Akizungumza jana kwa njia ya simu jana Sabas alisema Lema
anasababisha vurugu kwa kutembelea maeneo ambayo watu wamejitokeza na
kujiandikisha na kuanza kupiga hotuba kitu ambacho kinyume cha sheria.
Alisema Lema kama anataka kuhamasisha watu hatukatai, aende maeneo
ambayo daftari bado halijafika akahamasishe na likifika aache wananchi
wajiandikishe na siyo kuwafuata kwenye mistari na kuanza kupiga hatuba,
siyo sahihi.
Alisema polisi hawawezi kuonea mtu wala yeye mbunge, isipokuwa
likipata taarifa kama siku ya tukio ya Juni 20 alipokamatwa kuwa analeta
vurugu na wananchi hawataki kumwona katika maeneo ya uandikishaji ndipo
walipokwenda kumkamata.
Alisema siku ya tukio walipata taarifa toka kwa askari walioko doria
kwenye kituo cha Osunyai kuwa kuna vurugu toka kwa mbunge na kuomba
ulinzi uongezwe na askari wakapelekwa zaidi na kumtia mbaroni na wenzake
24 na kuwa jumla ya watuhumiwa 25 walikamatwa na siyo yeye aliyetoa
taarifa Polisi kuomba ulinzi.
“Lema yeye anaongozana na kundi la watu toka maeneo tofauti na
uandikishwaji, kitu ambacho siyo sahihi pia nacho kinakera baa- dhi ya
watu,” alisema.
Hata hivyo uchunguzi dhidi ya tuhuma zake unaendelea na upelelezi ukikamilika atachukuliwa hatua stahiki.
Awali Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, aliyekamatwa
alilalamikia Polisi, kwa kumkamata na kumweka mahabusu masaa kadhaa juzi
wakati akiwa kwenye kata ya Osunyai Manispaa ya Arusha, akizungukia
waandikishwaji wa daftari la wapiga kura, ili kujionea hali halisi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Lema alisema
ameshangazwa na kitendo hicho kwani yeye ndiyo aliyewaita polisi ili
kumsaidizi ulinzi, baada ya kuvamiwa kwa kupigwa mawe na kundi la vijana
wanaosadikiwa kuwa wa kundi la mgombea ubunge wa chama cha CCM.
Alisema mara baada ya kupiga simu Polisi kuomba msaada polisi
walifika kwa haraka, lakini badala ya kukamata vijana hao ambao walikuwa
wakizuia watu kujipanga mstari kwa madai siyo wakazi wa maeneo hayo kwa
madai wakazi wa maeneo hayo Wamasai na Waarusha, wakanikamata mimi na
wafuasi wangu 25 na kutuweka mahabusu.
Alisema walikaa ndani Juni 20 mwaka huu, kuanzia saa 1:30 usiku hadi
saa 4:00 usiku na kuwataka wajidhamini wenyewe, kisha kuwaachia.
Lema alisema yeye ni kiongozi na sheria inamtaka ahamasishe watu
kujitokeza na kujiandikisha na inapobidi kutoa elimu, lakini, hapaswi
kudhalilishwa kwa kuwekwa mahabusu kwa kejeli na dharau.
“Hawa watu wanaopita kwenye kata za wenyeji na gari aina ya Land
Cruiser yenye namba T.122 ATR na wakati mwingine hubadilisha kibao na
kusomeka T. 122 ABR, na kuwatoa watu kwenye mistari kwa madai siyo
wakazi wa maeneo hayo wakati wameuza maeneo na watu wamechanganyikana,
walipaswa wakamatwe, badala yake wanakamata mbunge na watu wake kuwa
wanahamasisha fujo, hiyo siyo haki,” alisema.