Suala la kuanza hedhi kwa watoto wa kike linasalia bado ni changamoto
katika nchi zinazoendelea, Tanzania ikiwa ni mojawapo. Inaelezwa kuwa
watoto wa kike baada ya kukabiliwa na mabadiliko ya mwili yanayoleta
hedhi, hukabiliwa na changamoto kama vile kukosa vifaa vya kujisafi na
hata ukaribu wa wazazi ili kuweza kuwasaidia. Je hali ikoje huko
Tanzania? Watoto wanapokea vipi mabadiliko haya? Basi tuungane na na
mwanahabari Neema Charles Mchacho wa mtandao wa wanahabari watoto kutoka
Mwanza nchini Tanzania, mtandao unaofadhiliwa na shirika la Umoja wa
Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.
No comments:
Post a Comment