Thursday, 4 June 2015

Moto waua 96 Accra Ghana

Mlipuko wa moto katika kituo cha mafuta, Accra Ghana umeua watu 96 na uchunguzi zaidi unaendelea.
Polisi wamezungushia uzio eneo hilo kwa sababu za usalama zaidi na kuchunguza idadi kamili ya watu waliopata madhara kutokana na mlipuko huo wa moto na kubaini chanzo chake. Hata hivyo mlipuko huo uliotokea baada ya mvua kubwa iliyosababisha mafuriko ya maji katika maeneo mengi ya mji wa Accra. Baadhi ya maeneo hayana umeme kutokana na kukatika kwa umeme,baadhi ya barabara hazipitiki kutokana na mafuriko hayo
Post a Comment