Kwa taarifa iliyotolewa kuhusu bunge la kutunga sheria, kuhusika na wimbi la mashambulizi dhidi ya albino ambapo sehemu ya mwili wake umekuwa ukiuzwa katika soko la Uchawi.
Naibu Waziri wa mambo ya ndani Perira Silima, alisema kuwa tuhuma za wanasiasa kuhusika na mauaji ya albino inaweza kuwa kweli kufuatia kufufuka kwa mashambulizi mapya dhidi ya albino mara baada ya mchakato wa uchaguzi kuanza.
Silima, aliwataka wanasiasa kutokuamini ahadi wanazopewa na waganga wa kienyeji.
Baadhi ya wanasiasi huamni ahadi wanazopewa kuhusu ushindi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika nchini Tanzania ifikapo mwezi Oktoba.
Perira, alisema kuwa "Nataka kuwahakikishia wanasiasa wenzangu kwamba hakutakuwa na kiti chochote bungeni ambacho kitachukuliwa kutokana na utumiaji wa viungo vya mwili wa albino"
No comments:
Post a Comment