Viongozi wa Jubaland pia waliishutumu serikali ya Somalia kwa kushindwa kuzingatia umuhimu wa mazungumzo ya makubaliano kama ilivyoelezewa kwenye katiba kuwa mojawapo ya njia za kutatua mizozo.
Siku ya Jumamosi, bunge la Mogadishu lilipiga kura kupitisha muswada na kutangaza serikali ya Jubaland kuwa inaenda kinyume na sheria.
Wanachama 132 kati ya 150 bungeni waliunga mkono na kupitisha muswada huo.
Baada ya uamuzi hatua hiyo, viongozi wa Jubaland wakatangaza rasmi kuvunja mahusiano yake na serikali ya Somalia.
No comments:
Post a Comment