Friday, 5 June 2015

Wananchi walalamikia ufinyu wa ukosefu wa vipimo na dawa katika zahanati wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Wananchi wa kijiji cha kiti cha mungu wilaya ya Mwanga mkoani kilimanjaro wamelalamikia tatizola ukosefu wa vipimo na dawa katika zahanati ya kijiji  hicho licha ya kuchangishwa fedha kiasi cha shilingi elfu kumi kwa ajili ya huduma za bima ya afya.
Wakizungumza na mwandishi wananchi wa kijiji hicho wamesema wanawake na watoto ndiyo wanateseka zaidi na kwamba wakifika katika zahanati hiyo hawapati huduma za afya badala yake wanapewa karatasi kwenda kununua dawa.
Wamesema kero hiyo inawakatisha tamaa ya kuendelea kuchagia fedha kwa ajili ya bima ya afya na kwamba wameshatoa malalamiko ngazi ya wilaya bila mafanikio hali inayowalazimu wananchi kutembea umbali wa zaidi km 10 kutafuta huduma za afya.
Kwa upande wake mganga wa zahanati ya kijiji cha kiti cha mungu Dkt.Chard  Mshana amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa dawa zinazoletwa katika kijiji hicho ni kidogo sana ikilinganishwa na idadi ya wananchi wanaohitaji huduma za afya.
Akijibu malalamiko hayo mkurugenzi wa halmashuri ya wilaya ya mwanga Bw.Jamuhuri Wilium ameahidi kufuatialia tatizo hilo na kulitafutia ufumbuzi kwenye  kamati za afya za wilaya ambazo zinahusika kusambaza dawa katika zahanati

No comments: