Nin ameunga mkono harakati za kupinga uamuzi wa Nkurunziza wa kutaka kugombea urais kwa muhula wa tatu ambao umezua utata na ghasia nchini Burundi.
Akitoa maelezo katika mkutano wa AU uliofanyika nchini Afrika Kusini, Nin alitoa wito kwa viongozi wa Afrika kumhimiza Nkurunziza kuachia ngazi ili kuepukana na ghasia zilizosababisha vifo vya watu wasiopungua 30 nchini Burundi.
Nin aliongezea kusema, ‘‘Mazungumzo yamecheleweshwa sana. Singependa kuona Umoja wa Ulaya ukichukua hatua kabla ya Umoja wa Afrika kwa sababu itakuwa ni aibu kubwa mno kwa bara la Afrika. Umoja wa Afrika utaonekana kuwa kama muungano usiokuwa na manufaa yoyote.’’
Suala la Nkurunziza na uchaguzi wa Burundi limejumuishwa katika ajenda ya mkutano wa AU lakini hadi kufikia sasa viongozi wanaonekana kutokuwa na matumaini ya kuibuka na ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment