Watalii hao wanne ambao wawili wamebainishwa kuwa raia wa Canada, mmoja wa Uingereza na mwingine mmoja wa Uholanzi, waliwabughudhi wananchi wa Malaysia kwa kujianika uchi juu ya kilele cha mlima Kinabalu.
Kitendo hicho cha utovu wa nidhamu kinaaminika kuudhi mapepo ya mlima Kinabalu na kusababisha maafa ya tetemeko la ardhi lililopelekea vifo vya watu 18 siku ya Ijumaa.
Watalii wote wanne walitakiwa kuchagua kati ya kulipa faini ya fedha dola 1,330 au kufungwa miezi mitatu gerezani iwapo watashindwa kulipa faini hiyo.
Uamuzi huo ulitoalea baada ya watalii hao kufungwa kwa siku tatu tangu siku ya Jumatano. Watalii hao pia wanatarajiwa kutimuliwa kutoka nchini humo.
No comments:
Post a Comment