Wednesday, 10 June 2015

Kocha mpya wa Simba atua Dar

Mrithi wa Kopunovic kutua DarSimba ipo mbioni kumpata mrithi wa Goran Kopunovic ambaye ni Didier Gomez de Roza raia wa Ufaransa anayetarajia kutua Tanzania mwishoni mwa wiki
SIMBA ipo mbioni kumpata mrithi wa Goran Kopunovic ambaye ni Didier Gomez de Roza raia wa Ufaransa anayetarajia kutua Tanzania mwishoni mwa wiki hii kwa ajili ya mazungumzo ya mwisho na kusaini mkataba.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ameiambia Goal kuwa wameshakubaliana mambo mengi ya kimsingi na kocha huyo na kilichobaki ni kuweka sawa baadhi ya mambo ili aweze kusaini mkataba na kuanza kazi ya kukinoa kikosi cha Simba.
“Nikocha mwenye rekodi nzuri ambazo tumevutiwa nazo na tukahisi atatusainia katika kurudisha heshima ya Simba ndiyo sababu ya kutaka kumchukua,”amesema Hans Poppe.
Simba iliamua kuachana na kocha wake Mserbia Goran Kopunovic aliyemaliza na timu hiyo msimu uliopita kutokana na kocha huyo kuhitaji kiasi kikubwa cha pesa ili aweze kusaini mkataba mpya kitu ambacho uongozi wa timu hiyo walishindwa.

No comments: