Monday, 8 June 2015

Mawaziri zidi ya 18 wangombania kuingia Ikulu

  1. Image result for kugombea urais tz 2015MBUNGE wa Bumbuli, January Makamba, ametangaza nia ya kuwania urais akisema kuwa Serikali yake itakuwa na mawaziri wasiozidi 18 wasiotiliwa shaka kwa kashfa zozote.

    January alitangaza nia hiyo Dar es Salaam jana. Alisema Serikali yake haitaundwa na mawaziri ambao ni waporaji na wabinafsi kwani kufanya hivyo kutaepusha masuala mbalimbali yasiyofaa yanayofanywa na watu wachache.Alisema hagombei nafasi hiyo ili kupambana na watu, bali kupambana na changamoto zinazowakabili Watanzania. ”Kugombea sio kugombana, hivyo kugombana hakumsaidii Mtanzania kuondokana na matatizo yetu,” alisema.Alisema akipewa ridhaa ya kuwa rais atatumia uwezo wake kuvunja makundi yaliyojitokeza katika  kipindi cha uchaguzi na kuwaunganisha wana CCM wote na kuwa kitu kimoja.

    January alisema kuwa akiwa rais hatokuwa na deni lolote la kulipa, hivyo hatopata kigugumizi kupambana na rushwa ikiwa ni pamoja na kufanya mabadiliko kwa taasisi ya TAKUKURU ili iwe na Mamlaka kisheria.

    Aliongeza kuwa ameamua kugombea nafasi hiyo kwa kuwa ana dhamira, uwezo, maarifa na ubunifu wa kukabiliana na changamoto zinazowakabili Watanzania. Mwanasiasa huyo kijana alisema serikali yake itaendeshwa na  falsafa ya uwezeshaji mpana wa wananchi ambapo pia itafumua mfumo mzima na kusuka upya uendeshaji Serikali kwa lengo la kuongeza uwajibikaji kwa kila mmoja.

    Alisema chini ya uongozi wake CCM itakuwa salama na kujenga Taifa la Watanzania ambapo kila mmoja atafurahia uongozi wake.

    January alitaja vipaumbele vyake kuwa ni pamoja na kukuza kipato cha watu, kuboresha huduma bora ili kuwa za uhakika, kuimarisha utawala bora, haki na sheria, usimamizi wa taasisi za  uchumi pamoja na ajira.
    Alisema Serikali yake haitokubali Mtanzania aonewe na mtu yoyote pamoja na kuhakikisha kila Mtanzania anatimiza wajibu wake. January alisisitiza kwamba Serikali yake itahakikisha kila ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) inapotolewa kama kuna taasisi imetajwa kwa ubadhirifu viongozi wa taasisi hizo wanatimuliwa kazi siku hiyo hiyo.

    Alisema akiwa rais asilimia 30 ya manunuzi ya Serikali yatapewa kampuni  zinazokidhi vigezo zitakazoendeshwa na vijana na wanawake. Alisema ndani ya miaka mitano atahakikisha viwanda 11 vya kutengeneza nguo vinajengwa  nchini na wanawake wakipewa kipaumbele katika suala la ajira.
    Aliongeza kuwa atahakikisha soko kuu la kitaifa la mazao linajengwa  litakalobadili hali ya maisha ya wakulima. Alisema kuwa katika elimu atahakikisha  kunakuwa na dira na malengo yatakayoongoza, uoanishaji wa mitaala.Alisema kuwa ndani ya uongozi wake atatoa sh.milioni 50 kwa kila kijiji ili kukopeshana.Alisema atahakikisha migogoro ya wakulima na wafugaji inamalizika kwa kuweka utaratibu wa ugawaji wa ardhi ambapo pia kutakuwa na mfumo wa satelaiti  ili kuangalia usalama wa nchi kwa ujumla na kumaliza migogoro ya ardhi.

    Kuhusu afya, alisema kila Mtanzania atakuwa na bima ya afya ili kuwawezesha kupata huduma za afya bila kujali vipato vyao pamoja na kuondoa urasimu katika Bohari Kuu ya Dawa.Akizungumzia usafiri wa reli, alisema utatumika mijini kumaliza tatizo la foleni kwa kushirikiana na sekta binafsi ambapo watajenga njia ya reli kutoka Bagamoyo  hadi Kibaha, Kisarawe hadi Kurasini.Alisema ili kutekeleza hayo yote  atahakikisha misamaha ya kodi isiyo na tija itapunguzwa hadi kufikia asilimia 1, kupanua wigo wa kodi.

No comments: