Viongozi wa kundi la mataifa
yaliyostawi zaidi kiviwanda G7, yamekata kauli kudumisha vikwazo
walivyoiwekea Urusi hadi pale taifa hilo litakapotekeleza kikamilifu
mkataba wa amani walioafikiana na Ukraine.
Uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao cha kila mwaka cha mataifa hayo tajiri.Chansela wa Ujerumani Angela Merkel amekariri kuwa vikwazo hivyo vimewekwa mahsusi ili kutatua tatizo hilo , na iwapo utawala wa Moscow utauendeleza mkataba huo wa amani basi bila shaka vitaondolewa.
Kwa mara ya pili tangu mzozo huo na Ukrain utokee rais Putin hakualikwa kwenye kikao hicho licha ya Urusi kuwa mwanachama wa G7.
No comments:
Post a Comment