Viongozi wa Ujerumani na Marekani wameweka msimamo mkali kwa
Urusi hii leo katika mkutano wa siku mbili wa kundi la nchi saba tajiri
duniani G7 unaofanyika nchini Ujerumani na uliogubikwa na mgogoro wa
Ukraine na Ugiriki. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa
Marekani Barrack Obama wametoa onyo kwa rais wa Urusi Vladimir Putin
kwa kile rais Obama alichosema ni uchokozi inaoufanya nchini Ukraine.
Viongozi hao wamekubaliana kuwa muda wa vikwazo unapaswa kufungamanishwa
na Urusi kutekeleza matakwa ya makubaliano ya amani ya Minsk na
kuheshimu uhuru wa Ukraine. Mkutano huo wa G7 unaohudhuriwa pia na
viongozi kutoka Uingereza, Canada, Ufaransa, Italia na Japan
utazungumzia kwa kina masuala ya uchumi wa dunia, ugaidi, umaskini
pamoja na mabadiliko ya tabia nchi
No comments:
Post a Comment