Thursday, 26 June 2014

Al shabaab Washambulia tena hotel


Wanajeshi wa Amisom nchini Somalia
Taarifa kutoka Somalia zinasema kwamba kumekuwa na makabiliano makali milipuko na milio ya risasi ikisikika katika eneo la hoteli moja inayotumika kama makao makuu ya vikosi vya Afrika vya kulinda amani.
Walioshuhudia shambulizi hilo wanasema hoteli hiyo iliyopo katika mji wa Bulo- burde, umeshambuliwa na wanamgambo wa Al -shabaab.
Hoteli hiyo inayotumiwa na wanajeshi wa Muungano wa Afrika AMISOM,pamoja na jeshi la Somalia katika eneo la Buuloburde, kati kati mwa Somalia ililengwa kwa mashambulizi na wapiganaji wa Al Shabaab.
Kundi hilo limekiri kufanya mashambulizi hayo, na kuongeza kwamba wamewaua angalau wanajeshi sita wa Amisom.
Msemaji wa Amisom alisema kuwa wanajeshi wake watatu wameuawa katika shambulizi hilo.
Wapiganaji wawili waliokuwa wamevalia magwanda ya kijeshi,walivamia hoteli hiyo na kuanza kuwapiga risasi wanajeshi. Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa walisikia milio ya risasi kwa muda wa saa moja na nusu kabla ya wanajeshi hao kuwaua washambuliaji.
AMISON ilidhibiti eneo la Buuloburde mwezi Machi, lakini mji huo unasema kuwa al shabaab imezuia barabara zote kuelekea katika hoteli hiyo.
Wanajeshi wa Amisom, wanaweza tu kupata mahitaji yao kwa kutumia ndege.Wakazi wengi walitoeoka mjini humo na sasa wanaishi viungani wa mj wenyewe.

No comments: