Bonanza la kuapishwa kwa Mawaziri
wa chuo kikuu cha maendeleo ya jamii Tengeru limefanyika leo hukulililokuwa limegubikwa na
michezo ya aina mbali mbali kama vile ukimbizaji wa kuku,Volleyball(mpira wa
wavu) na Mpira wa miguu .Katika Bonanza hilo mawaziri walio apishwa ni pamoja
na waziri wa Elimu (Erick Eponda) Afya na Mazingira (BeatriceKaranja ) Michezo na utamaduni (Emmanuel na naibu wake Goodbless Lema naLoserian
Moleli, Sheria na Katiba (Lule ) waziri wa Mikopo Makali Lyaki na naibu wake ni Loserian Molel.
Katika
uapishwaji huo mchezo ulio wavutia wengi ni mpira wa miguu ambao ulishindanisha
Timu toka chuo hapa Chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru (TICD) na timu alikwa
toka chuo cha Kilimo Tengeru (LITA)
Katika Mchezo huo ulio pigwa
katika kiwanja cha Chuo cha LITA ulikuwa ni wakusisimua na wenye mvuto ambapo
kila timu iliingia uwanjani zikiwa zimekamiana na kila timu ikihitaji ushindi
Kipindi cha kwanza kilianza kwa
kasi huku timu zote mbili zikiwa zinalisakama lango la mwenzie mnamo dakika ya
40 ya mchezo nusura LITA wajipatie bao la kuongoza baada ya kiungo mkabaji wao
kupiga shuti lililomshinda mlinda mlango wa TICD na kugonga mwamba hadi mapumziko
TICD 0 0 LITA
Kipindi cha pili kilianza kwa
kasi huku Timu ta TICD ikianza kwa kasi na kwakushambulia lango la LITA huku
mshambuliaji wa TICD Goobless Lema akionekana Mwiba kwa mabeki wa Lita , Mnamo
Dakika ya 68 Mshamuliaji hatari Goodbles Lema alitoa pasi ya mwisho kwa
Herndricos Twinzi alimaarufu kwa jina la Chicharito na
kutumbukiza mpira nyavuni na kufanya TICD kiongoza kwa bao 1
Hata hivyo LITA haikukata tama
ilijikakamua na kulishambulia lango la TICD mara kwa mara bila Mafanikio ,,
Mnamo dakika ya 72 ya mchezo TICD walifanya mabadiliko kwa kumtoa Sixbert jezi
namba 9 na kumwingiza Deogratius jezi namba 14 . Mabadiliko haya yaliongeza
ladha ya mpira na kufanya mpira uwe wa kazi na wakushambuliana kwa zamu
Mnamo dakika ya 85 LITA
walielekeza mashambulizi makali kwenye lango la TICD mshambuliaji Elia wa LITA
alitoa pasi kwa mshambuliaji hatari wa LITA aliyekuwa akiisumbua ngome ya TICD
kwajina alifahamika kama Kabamba aliyepiga shuti na kupaa sentimita chache juu
ya lango la TICD ambapo mwamuzi wa mchezi huo alishindwa kuona vyema na kuamuru
kuwa ni goli , Hata hivyo washika vibendera walipingana na mwamuzi wa kati na kupelekea mwamuzi huyo kubadili
mawazo yake na kusema mpira upigwe kama kona ambapo wachezaji wa LITA
walipingana na mawazo ya mwamuzi huyo na kuleta vurugu ambapo ulipelekea mchezo
kuvunyika mnamo dakika ya 87 , Hadi kuvunjika kwa mchezo TICD 1 0 LITA
No comments:
Post a Comment