Waziri wa maswala ya kigeni
nchini Marekani JohnKerry yupo mjini Cairo nchini Misri ili kukutana na
rais mpya wa Misri Abdul Fatah Al Sisi.
Ni Mwanasisa wa hadhi ya juu kuzuru nchini Misri
tangu kamanda huyo wa zamani wa jeshi kuchaguliwa kama rais baada ya
kumpindua aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi.Maafisa wa Marekani wanasema kuwa bwana Kerry yuko nchini humo kumtaka rais Al sisi kuwashirikisha watu wote katika siasa yake ikiwemo wanachama wa kundi la Muslim Brotherhhod lililopigwa marufuku.
Kerry pia anatarajiwa kuzungumzia kuhusu hukumu ya kifo iliotolewa dhidi ya wanachama wengi wa kundi hilo mbali na kutoa wito wa kuachiliwa kwa waandishi waliofungwa.
Waandishi walio katika ziara hiyo ya bwana kerry amesema kuwa Marekani iko tayari kuanzisha mazungumzo na rais huyo mpya ikiwa na matumaini kwamba mazungumzo hayo yataleta natija.
No comments:
Post a Comment