Sunday, 22 June 2014

Jose Mourinho asema England hawana cha kulaumu kwa kutolewa katika kombe la Dunia

England haina haja kusikia aibu yeyote kwa kutolewa mapema kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil kwa mujibu wa Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho.
England, wakicheza Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia, walifungwa Mechi zao zote mbili za kwanza na Italy na Uruguay, zote kwa Bao 2-1 kila moja, na wamebakisha Mechi moja dhidi ya Costa Rica ambayo kwao ni kukamilisha Ratiba tu.
Mara ya mwisho kwa England kushindwa kuvuka hatua ya Makundi ni Mwaka 1958.
Lakini Mourinho amewapa moyo kwa kusema: “Sisikii vizuri kuiponda England kwa sababu hawastahili kusikia aibu kwa hili. Hawakuwa na Miungu ya Soka upande wao!”
Mourinho anaamini England walipewa kazi ngumu sana walipowekwa Kundi moja na Italy na Uruguay.
Kocha huyo kutoka Uremo alisema: “England hawakuwa na bahati. Imetokea Kundi lao lina Mabingwa wa Dunia Watatu ambao ni Uruguay, Italy na England. England walicheza vizuri, walishindana vizuri, hawakuziogopa Italy wala Uruguay!”
Jumanne Juni 24 England watacheza na Costa Rica ambayo tayari imetinga Raundi ya Pili ya Mtoano.
KOMBE LA DUNIA-Brazil 2014
MSIMAMO:

KUNDI D
TIMU P W D L F A GD PTS
Costa Rica 2 2 0 0 4 1 3 6
Italy 2 1 0 1 2 2 0 3
Uruguay 2 1 0 1 3 4 -1 3
England 2 0 0 2 2 3 -1 0

No comments: