Akizungumza na mwandishi wetu hili Dar es Salaam jana,
Jasmin alisema jambo la kwanza atakalofanya ni kurudisha nguvu ya umoja
wa wanawake wa Simba kwa kufanya nao kazi kwa karibu.
“Umoja wa wanawake ni muhimu katika klabu yetu
kwani ni nguzo muhimu katika maendeleo ya Simba, lakini kwa siku za
karibuni kundi hili limekuwa nyuma,” alisema.
Mgombe huyo alijinadi kuwa atalinda katiba ya
Simba na kudumisha uhusiano mzuri baina ya matawi na wanachama wote wa
klabuni hapo.
Alisema kwa kipindi cha miaka saba aliyofanya kazi
kama katibu muhtasi wa klabu hiyo, amejifunza mengi na atakuwa mshauri
mzuri kwa rais ajaye iwapo atachaguliwa kuwa mjumbe katika Kamati ya
Utendaji, huku mkazo wake ukiwa katika soka.
Jasmin, ambaye ni mke wa beki wa zamani wa Simba,
Victor Costa alibainisha kuwa maneno bila vitendo katika klabu yoyote ya
soka, ni kujidanganya kwani mwisho wa siku soka linatakiwa lionekane.
“Simba kama klabu haiwezi kuwa imara bila
kuhakikisha mpira unachezwa kwa kiwango cha juu uwanjani, hivyo ili
kuhakikisha hilo linatimia ni vema kuchagua viongozi wa mpira na si wa
maneno.
“Chagueni viongozi wapenda mpira, msichague
wapenda ofisi na majigambo. Wapenzi na wadau wa soka hawataki maneno
wanataka mpira siyo tu kuwapo bali kuonekana unachezwa kwa kiwango na
hadhi ya timu yenye miaka mingi kama Simba,” alisema.
Jasmin aliongeza kuwa wakati wa kucheza soka la
kelele na fitina umekwisha kutokana na kuwapo kwa upinzani wa kweli
kwenye soka, hivyo wanachama wanapofanya uchaguzi walitilie maanani
suala hil
No comments:
Post a Comment