Jenerali muasi anusurika shambulizi la Bomu |
Mlipuaji wa kujitioa mhanga
ameshambulia nyumba ya jenerali muasi ambaye amekuwa akiongoza kampeni
za kijeshi dhidi kundi la wapiganaji wa kislamu wanaoungwa mkono na
serikali nchini Libya ambao watu wanne waliuawa.
Jenerali Khalifa Haftar alinusurika shambulio
hilo lililotekelezwa kwenye jengo moja la shambani kwenye mji wa Abyar
karibu kilomita sitini mashariki mwa Benghazi.Watu kadha walijeruhiwa.
Vikosi vya Jenerali Haftar vimekuwa vikiendesha kampeni dhidi ya wapiganaji wa kiislamu mjini Benghazi kwa kipindi cha majuma matatu sasa.
Haftar ambaye alikuwa mkuu wa majeshi wakati wa utawala wa rais wa zamani Muammar Gaddafi anaishutumu serikali kwa kuunga mkono ugaidi madai yanayokanushwa na serikali.
Jenerali Sager AL-Jarushi ambaye ni kamanda wa ngazi za juu na mshirika wa karibu wa Jenerali Haftar aliwambia waandishi wa habari kuwa wanne kati ya walinzi wake waliuawa kwenye shambulizi hilo.
Watu wengine 20 wanaripotiwa kuuawa kwenye mapigano makali kati ya vikosi vya Jenerali Haftar na wapiganaji wa kislamu mjini Benghazi .
No comments:
Post a Comment