IVO Mapunda wa Simba, amesema kuanzishwa
kwa timu ya umoja wa makipa Tanzania, umemaliza tofauti za walinda
mlango wote na sasa yeye pamoja na Juma Kaseja na Ally Mustapha
‘Barthez’ ni kitu kimoja.
Awali kulikuwa na minong’ono kuwa makipa hao hawana maelewano mazuri kutokana na sababu mbalimbali za ndani na nje ya Uwanja.
Lakini sasa walinda mlango hao, wanakula,
wanakunywa na kufanya mazoezi kwa pamoja kila siku nyakati za asubuhi na
jioni kwenye Uwanja wa Gadren, Kinondoni.
Ivo alisema: “Tunapokuwa kwenye timu yetu hii,
watu huwa wanasubiri waone kitatokea nini baina yetu, lakini wanashangaa
kuona tupo kwa pamoja na amani. Tunashirikiana kwa kila jambo kama
kupongezana kwa mambo mbalimbali kama unavyojua tunakuwa timu moja,
tunapata mialiko kwenda sehemu mbalimbali, tunakula na kunywa
pamoja,”alisema Ivo na kuwataka wadau wajititokeze kuidhamini timu yao
kwani wanajiongoza na kujitegemea wenyewe kwa kila kitu kwa sababu ya
kukosa mfadhili.
“Hata ile imani ya kwamba sisi hatuelewani huwa ni
mashabiki wenyewe tu lakini siyo sisi. Tunafanya mazoezi mara mbili
ambapo asubuhi huwa tunafanya yetu ya ukipa na jioni, tunafanya ya
kucheza uwanjani kama unavyojua hii ni timu ya wachezaji 11 wanaocheza
ndani kama zilivyo nyingine za soka.”
Baadhi ya makipa ambao wapo na kikosi hicho ni pamoja na Shaaban Hassan ‘Kado’, Kaseja, Barthez, Ivo, Jackson Chove na wengineo.
No comments:
Post a Comment