Ilichukua dakika 26 tu kwa Algeria kupata goli lake la kwanza kupitia
kwa Slimani kabla ya Halliche kutia goli la pili kimyani dakika mbili
mbele. Haikuchukua muda mrefu zaidi kabla ya kupata goli la tatu katika
dakika ya 38.
Kipindi cha pili kilikuwa na mikikimikiki mingi zaidi. Korea
walijaribu kupunguza magoli na kupata goli la kwanza katika dakika ya
50. Hata hivyo Algeria walizidisha wimbi la magoli kwa kufunga goli
katika dakika ya 62. Dakika ya 72 Korea walipata goli la pili na la
mwisho.
No comments:
Post a Comment