BUNGE Maalum la Katiba limepata pigo baada ya kuondokewa na mjumbe wake, Shida Salum (64), ambaye ameugua kwa muda mrefu.
Shida ambaye pia ni mama mzazi wa mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe
Zitto (Chadema), amesumbuliwa na maradhi ya saratani ya shingo ya kizazi
na hivyo kushiriki vikao vya awali pekee vya utungwaji wa kanuni za
Bunge hilo.
Kwa mujibu wa Zitto, mama yake ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya
Chadema Taifa na Mwenyekiti wa Watu wenye Ulemavu nchini, alikumbwa na
mauti saa tano asubuhi jana hospitalini hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari, muda mfupi kabla ya sala ya
kuombea maiti katika Msikiti wa Maamur ulioko Upanga, Zitto alisema mama
yake alizaliwa Julai 1950 na kusoma shule ya sekondari Tabora.
Kwa mujibu wa mbunge huyo, mama yake alikuwa akisumbuliwa na saratani
ya shingo ya kizazi ambapo amepata matibabu katika hospitali za ndani
na nje.
Shida ambaye pia alikuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ameacha watoto 10 ambapo sita ni wakiume na wanne ni wa kike.
Akizungumzia taratibu za kibunge, Katibu wa Bunge Dk. Thomas
Kashilila alisema kifo cha mtu ambaye si mbunge taratibu za mazishi
hushughulikiwa na familia.
Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano), Steven Wassira alisema Shida alikuwa mwanasiasa anayelipenda taifa lake.
Mwili huo ulisafirishwa jana kwenda mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi yatakayofanyia leo eno la Mwanga.
No comments:
Post a Comment