Frank Lampard |
NI kama hadithi, lakini wala haiwezi kushangaza sana kumwona kiungo, Frank Lampard, akikaribia kuvaa jezi ya Manchester City licha ya awali kuahidi kutovaa jezi ya timu nyingine yoyote zaidi ya Chelsea.
Habari kutoka England zinadai kwamba matajiri wa
Manchester City ambao wamemnunua Lampard akachezee timu yao ya New York
City ya Marekani, wanataka aichezee City kwa mkataba wa muda mfupi.
Mkataba wa Lampard Stamford Bridge umemalizika
mwezi huu na yupo huru kujiunga na klabu yoyote anayoipenda baada ya
Chelsea kuamua kutomwongezea mkataba mwingine kama ilivyo kwa Ashley
Cole.
Ligi Kuu Marekani itaanza Machi mwakani na
Manchester City wanataka Lampard asaini mkataba wa miezi sita kwa ajili
ya kuichezea timu yao ya Etihad mpaka wakati huo.
Wiki tatu zilizopita, Lampard, ambaye atatimiza
umri wa miaka 36 mwezi huu, alidai kwamba kamwe asingeweza kuvaa jezi ya
timu nyingine na kucheza mechi dhidi ya Chelsea, lakini matajiri wa
City wana matumaini kwamba Lampard atabadili mawazo kwa ajili ya
kuongeza wachezaji Waingereza.
Wachezaji watano raia wa Uingereza; Micah
Richards, Jack Rodwell, Gareth Barry, Scott Sinclair na Joleon Lescott,
wote wanatazamiwa kuondoka katika dirisha hili na Manchester City iko
hatarini kupoteza msingi wake wa wachezaji wa taifa hilo.
Lampard, ambaye juzi Jumapili alipaa na kikosi cha
England kwenda Miami kwa ajili ya kujiandaa na fainali za Kombe la
Dunia huku akiwa kama kocha msaidizi, ataungana na mshambuliaji wa
Atletico Madrid, David Villa katika klabu ya New York City.
No comments:
Post a Comment