|
Ndege ya Malaysia ikiitafuta meli iliyoweka |
Serikali ya Australia imetangaza eneo jipya la kuitafuta
ndege ya abiria ya Malaysia iliyotoweka na zaidi ya abiria 200 mwezi
Machi mwaka huu.
Naibu Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Warren Truss amesema baada ya
wataalam kuthathmini upya ni wapi ndege hiyo inawezakuwa iliangukia,
eneo hilo jipya ni Kilomita 1,800 Pwani Magharibi wa Australia.
Ndege hiyo ya abiria MH370
ilitoweka ghafla ikielekea jijini Beijing nchini China ikitokea jijini
Kuala Lumpur nchini Malaysia ikiwa na abiria 239 wengi wao wakiwa
raia wa China.
Wataalam wanasema kuwa baada ya uchunguzi wao wamebaini kuwa ndege hiyo ilikuwa haindeshwi na rubani ilipozama.
Ripoti ya serikali ya Australia yenye ukurasa 64 imependekeza kuwa utafutaji huo ufanyika katika eneo la Kilomita 60,000 mraba.
|
Meli maalum ya Marekani ikiitafuta ndege ya Malaysia |
Mwezi Aprili, Mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Marekani yalituma
meli maalum za majini kujaribu kuitafuta ndege hiyo sakafuni mwa bahari
bila mafanikio.
Utafutaji wa ndege hii ndio ghali zaidi katika historia ya utafutaji
wa ndege ya abiria iliyopotea katika mazingira ya kutatanisha.
Familia za abiria waliotoweka baada ya kupotea kwa ndege hiyo
wanasema wameghabishwa na kutopatikana kwa mabaki ya ndege hiyo ambayo
hadi sasa haijulikani ilipo.
No comments:
Post a Comment