Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo imesisitiza kupokonywa silaha waasi wote wa Rwanda walioko
nchini humo. Lambert Mende Omalanga, Waziri wa Habari na msemaji wa
serikali ya Kongo amesema leo kuwa, serikali ya Kinshasa ipo tayari
kuwapa fursa nyingine waasi wa Rwanda wa FDLR ili waweke silaha zao
chini. Omalanga ameongeza kuwa, iwapo waasi hao hawatajisalimisha
wenyewe katika muda utakaopangwa, serikali ya Kongo itafanya operesheni
ya kuwapokonya silaha kwa nguvu. Waasi 100 wa Kihutu Mei 30
walijisalimisha na kukabidhi silaha zao huko Mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo.
Licha ya kusambaratishwa kundi la waasi
wa M23 lililokuwa likihesabiwa kuwa muhimu zaidi nchini humo, lakini
bado amani na utulivu haujaimarishwa kikamilifu nchini Kongo kutokana na
kuwepo makundi mengine ya waasi na ya upinzani.
No comments:
Post a Comment