Friday 20 June 2014

Wafungwa watoroka jela

Wafungwa 15 watoroka gerezaniWafungwa 15 walifanikiwa kutoroka gerezani mjini Bamako, Mali.

Wafungwa 15 kati ya 23 waliojaribu kujikomboa kutoka gereza kuu mjini Bamako wafanikiwa kutoroka huku wenzao 8 wakikamatwa.
Mfungwa mmoja na mlinzi mmoja wa gereza hilo waliaga dunia katika makabiliano yaliyozuka katika mchakato wa kutoroka.
Katibu Mkuu katika wizara ya sheria nchini humo Boya Dembele alisema kuwa wafungwa hao walipata fursa ya kutoroka wakati vyumba vyao vilipokuwa vikikarabatiwa. Dembele aliongezea kuwa wafungwa 8 waliokuwa wametoroka walikamatwa na wananchi waliokuwa wakiwasaidia askari kuwatafuta. Dembele alisema kuwa polisi wanaendelea na msako wao wakuwatafuta wafungwa hao. 

No comments: