Saturday, 7 June 2014

Nchi zilizoendelea bado kutimiza ahadi ya kuchangia mfumo wa mabadiliko ya tabianchi


Upandaji miti unasaidia kufyonza hewa ya ukaa inayosababisha ongezeko la joto duniani.

Wakati Mkutano kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi ukiendelea leo mjini Bonn, Ujerumani kwa ajili ya kuandaa mkataba mpya wa mabadiliko ya tabianchi hapo mwakani, mwenyekiti wa kamati ya dunia ya kisayansi na taaluma ya mkataba kuhusu makubaliano ya hali ya hewa, UNFCCC, Richard Muyungi, amezungumza na idhaa hii kuhusu mwelekeo wa mkataba huo mpya.
Amesema, bado ahadi zilizotolewa Kyoto kwa ajili ya kusitisha ongezeko la joto duniani, hazijatekelezwa.
(Sauti Muyungi-1)
Pia ameeleza msimamo wa nchi zinazoendelea katika mazungumzo hayo.
(Sauti Muyungi-2)
Muyungi amesema nchi zilizoendelea zimeahidi kufadhili mfuko mpya wa mabadiliko ya tabianchi kwa kiasi cha dola bilioni moja kwa mwaka, lakini hadi sasa, mfuko huo haujafadhiliwa hata senti tano.

No comments: