Monday, 2 June 2014

Peter Mutharika akabidhiwa madaraka leo

Rais Mutharika akikagua gwaride katika uwanja wa Kamuzu

Maelfu ya watu wamehudhuria sherehe za kukabidhiwa mamlaka kwa Rais mpya Peter Mutharika.
Bwana Mutharika, alishinda uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi jana. Uchaguzi huo ulikumbwa na madai ya wizi wa kura.
Rais anayeondoka mamlakani Joyce Banda, alishika nafasi ya tatu katika idadi ya kura za urais.
Viongozi kadhaa kutoka Afrika walihudhuria sherehe hizo katika uwanja wa Kamuzu, mjini Blantyre.
Mtangulizi wake Mutharika, Joyce Banda alisusia sherehe hizo.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza ambaye yuko mjini Blantyre, anasema kuwa serikali ilitoa mwaliko kwa wakuu wa nchi kadhaa za Afrika wakiwemo majirani zake wote ili kushuhudia hafla hiyo muhimu.
Jumamosi asubuhi Jaji mkuu Anastazia Msosa alimwapisha Mutharika kuwa Rais wa tano wa Malawi ikiwa ni saa 12 tu baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliokuwa umejaa malalamiko ya wizi wa kura na mapingamizi mahakamani.
Akizungumza nyumbani kwake mara baada ya kula kiapo Rais Mutharika amewaahidi wamalawi uhudumu bora na kumaliza kiu yao ya maendeleo, huku akiwataka wapinzani wake katika mbio za urais akiwemo Dr Joyce Banda waungane naye kuijenga Malawi.
Dr Banda pamoja na wagombea urais wengine kumi na moja walioshindwa, wamempongeza Rais mpya na kuwataka wafuasi wao kukubali matokeo na kujipanga upya kwa uchaguzi ujao wa mwaka 201

No comments: