Monday 2 June 2014

CHADEMA yatoa salamu za rambirambi kwa zito

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeeleza kupokea kwa majonzi makubwa msiba wa mjumbe wao wa Kamati Kuu ya Taifa, Shida Salum ambaye aliaga dunia jana jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya CHADEMA iliyotolewa na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, Shida ambaye vile vile ni mama mzazi wa mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA) na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ameacha pengo kubwa kutokana na utumishi wake wa muda mrefu ndani ya chama.
“Kwa niaba yangu binafsi na chama changu napenda kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya mama Shida. Tunaungana na familia katika wakati huu mgumu japo tumepokea taarifa za kuondokewa na mama yetu tukiwa tumetawanyika katika maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya shuguli za chama,”alisema.
Mbowe alisema kuwa kutokana na uharaka wa mazishi yanayotarajiwa kufanyia leo mkoani Kigoma, amemteua mjumbe wa Kamati Kuu, Ezekiel Wenje ambaye pia ni mbunge wa Nyamagana kuwakilisha chama katika mazishi hayo huku viongozi wengine nao wakijaribu kutafuta usafiri kwa njia yoyote kujaribu kuwahi mazishi.
“Wenje tayari tumemkodishia ndege ya kwenda Kigoma, kwa sababu yeye alikuwa Dar es Salaam kutuwakilisha pia hospitalini wakati mama Shida akiugua na alikata roho akiwepo hapo. Lakini mimi pia huku Kilimanjaro najaribu kutafuta usafiri wowote kuona kama nitawahi mazishi hayo,”alisema.
Akimzungumzia marehemu, Mbowe alisema kuwa atakumbukwa daima kwa kukipigania chama chake, pamoja na familia yake kwa muda wote wa maisha yake.
Hata hivyo, Mvungi licha ya kushiriki vikao vilivyopanga mazishi ya Nasra, jana alisema angefurahi kama angepewa mwili wa mtoto wake ili auzike mwenyewe badala ya kuzikwa na Serikali.
“Tayari mimi na familia yangu akiwamo mke wangu tulishakubaliana kumlea na nilipanga baada ya kupona niwaombe ustawi wa jamii ili nimlee mwenyewe, lakini leo nilipopata taarifa hizi kwa kweli nimechanganyikiwa na sijui cha kufanya.’’
Katika kikao cha mazishi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi ya Al Saed, Omary Al Saed alisema kampuni yake itatoa gharama zote za mazishi kuanzia kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Morogoro na gharama nyingine.
Wadau wengine ambao walitoa michango yao ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Morogoro (MRFA), Pascal Kianga na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.
Mateso ya Nasra
Nasra alifichwa katika boksi na mama yake mkubwa, Mariam Said mkazi wa Uwanja wa Ndege, Morogoro tangu akiwa na miezi tisa.
Alianza kumlea mtoto huyo baada ya mdogo wake ambaye ni mama yake Nasra kufariki dunia. Majirani wa Mariam ndiyo waliotoa taarifa za kuwepo kwa mtoto huyo baada ya kumsikia akilia na kukohoa nyakati za usiku.
Mwanamke huyo, Mvungi na mume wa Mariam, Mtonga Omar wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Morogoro kujibu mashtaka ya kula njama na kufanya ukatili dhidi ya mtoto huyo.
Jana Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, John Laswai alisema kutokana na kifo cha Nasra, mashtaka dhidi ya watuhumiwa yanaweza kubadilika, lakini mabadiliko hayo yatategemea ripoti ya daktari kuhusu sababu za kifo hicho.
Laswai alisema taratibu za kipolisi zinafanywa kuwezesha  kupatikana kwa taarifa hiyo, ambayo itapelekwa kwa wanasheria ambao baada ya kuipitia wanaweza kuwa na mapendekezo ya kubadili mashtaka dhidi ya watuhumiwa hao.

No comments: