Kongamano la siku tatu kuhusu nishati endelevu kwa wote limeanza leo
hapa New York, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Joshua Mmali na
taarifa kamili
Taarifa ya JOSHUA
Kongamano hilo linawaleta pamoja wadau kutoka
mashirika mseto ya ubia, likilenga kuongeza kasi ya uchukuaji hatua
katika sekta ya biashara na serikalini, kuchagiza ushiriki wa mashirika
ya umma na vijana, pamoja na kuongeza upatikanaji wa nishati endelevu
kwa kuwawezesha wanawake.
Washiriki kwenye kongamano hilo pia wanaangazia
masuala ya kuchagiza uwekezaji katika nishati endelevu kupitia mifumo
bunifu ya biashara, na kwa kubadilishana ujuzi na uzoefu. Mmoja wa
washiriki ni Mariam Mohamed Abdallah, wa shirika la Youth Climate
Movement
Sauti ya Mariam
"Uendelevu
unahusu elimu, upatikanaji wa rasilmali, na kadhalika, lakini
tunapozungumzia umaskini na utulivu, tunaangalia umaskini wa nishati. Ni
lazima tuutokomeze umaskini wa nishati, kwa njia endelevu, kwa sababu
umaskini wa nishati na umaskini wa rasilmali kwa ujumla, huchangia
migogoro na kutishia utulivu, na hivyo kuharibu mazingira ya maendeleo
na uendelevu."
Hapo kesho, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
anatarajiwa kulihutubia kongamano hilo, ambapo pia atazindua rasmi
Mwongo wa Umoja wa Mataifa wa Nishati Endelevu kwa Wote
No comments:
Post a Comment