
Mwandishi wa habari kijana wa Somalia ameuwawa kwenye mripuko wa bomu lilotegwa chini ya gari lake mjini Mogadishu.
Yusuf Keynan alikufa wakati bomu hilo liliporipuka alipotia moto gari, akitaka kuelekea kazini.
Mwandishi wa habair mjini Mogadishu
wanasema Yusuf Keynan (aliyefanya kazi katika redio Mustaqbal), alikuwa
mwandishi wa habari kijana aliyekuwa akipendwa na hodari katika kazi
yake.
Huyo ni mwandishi wa habari wa kwanza kuuwawa
nchini Somalia mwaka huu, baada ya waandishi habari kadha kuuwawa kwa
mfululizo katika miaka miwili iliyopita.
Shirika la Kuwalinda Waandishi wa Habari linasema kuwa Somalia ni moja kati ya nchi hatari kabisa kwa waandishi.
Hakuna aliyedai kuhusika na mauaji ya kijana huyo
No comments:
Post a Comment